Kitaifa

Mkude Akimbizwa Muhimbili kwa Matibabu Zaidi

on

NAHODHA wa timu ya Simba Jonas Mkude amekimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupata ajali ya gari aina ya Toyota Land Cruiser maeneo ya Dumila Mitibora mkoani Morogoro akitokea Dodoma katika mchezo wa fainali ya kombe la FA ambayo waliibuka mabingwa.

Gari hilo lenye namba za usajili T 834 BLZ lilipasuka mpira wa nyuma hali iliyosababisha kuacha njia na kuingia porini ambako lilipinduka mara kadhaa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo Mkude amepata majeraha kichwa lakini wanawake wawili kati ya watu sita waliokuwemo ndani ya gari hilo ambao majina yao hayakupatikana mara moja hali zao sio nzuri na wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa Morogoro.

Mkude ambaye alipelekwa hospitali Morogoro kupata huduma ya kwanza,  alitumia usafiri huo binafsi kwa ajili ya kuwahi kambi ya timu ya Taifa ambayo wanatarajia kuondoka nchini keshokutwa kuelekea nchini Misri kwa kambi ya wiki moja.

Jonas Mkude

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *