The sports Hub

Mnaozungumzia Ubingwa Ligi Kuu Msikilizeni Ajibu

0 632

NAHODHA na Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amewapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia ni mapema kukata tamaa ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kwamba bado wana nafasi ya kulichukua taji hilo.

Mkali huyo wa kuuchezea mpira alisema bado mechi nyingi zimebaki kwao na watani wao Simba, hivyo haoni sababu ya kukata tamaa ya kulichukua taji hilo.

”Sare tuliyoipata dhidi ya Singida United imewakatisha tamaa baadhi ya mashabiki kuchukua ubingwa wa ligi kuu,’hii sio sahihi kwani bado safari ni ndefu sana, tuna nafasi ya kutwaa taji hili’ alisema Ajibu.

Mchezaji huyo alizidi kufafanua kuwa kutokana na idadi ya mechi zilizosalia bado hakuna timu iliyojihakikishia kuchukua ubingwa huo. Hadi sasa Yanga ndio inayoongoza ligi ikiwa na pointi 55, huku Simba ikiwa na pointi 36 na faida ya mechi saba za viporo.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.