Kimataifa

‘Mnyama’ Ronaldo Awazima Wenyeji Urusi Mabara

on

MOSCOW, Urusi
BAO la mapema la mshambuliaji Cristiano Ronaldo limetosha kuipa ushindi Ureno baada ya kuwafunga wenyeji Urusi katika michuano ya kombe la mabara inayoendelea nchini humo.

Ronaldo alifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya nane baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Raphael Guerrero upande wa kushoto huku mabeki wa Urusi wakishindwa kuokoa hatari hiyo.

Ureno ilimiliki zaidi mchezo kipindi cha kwanza kwa kufanya mashambulizi mengi langoni mwa wapinzani wao kabla ya wenyeji kubadili upepo kipindi cha pili lakini safu ya ulinzi iliyokuwa chini ya Pepe na Bruno Alves ilikuwa imara kumlinda golikipa wao Rui Patricio.

Ureno wanaongoza kundi A wakiwa na alama nne kufuatia sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mexico huku Urusi ikiwa ya pili na alama tatu baada ya kuifunga New Zealand mabao 2-0.

Katika mchezo wa pili wa kundi hilo utakaochezwa muda mfupi kutoka sasa Mexico itashuka dimbani kuikabili New Zealand.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *