The sports Hub

Mo Salah Akataa Tuzo, Aelekeza Iende kwa Milner

0 133

STRAIKA wa Liverpool Mohamed Salah amekataa kupokea tuzo ya mchezaji bora wa mechi (Man Of The Match) na kutaka zawadi hiyo apewe mchezaji mwenzake James Milner ambaye emefikisha idadi ya mechi 500 katika Ligi Kuu ya Uingereza leo.

Salah alitunukiwa zawadi hiyo baada ya kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bournemouth huku yeye akifunga mabao matatu (hat-trick)katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Vitality.

Salah amesema kuwa ameelekeza tuzo hiyo ikabidhiwe kwa Milner kama sehemu ya heshima na kutambua uwezo wake pamoja na uwepo wake katika ligi hiyo hadi kufikisha mechi 500.

Ikumbukwe hiyo ni hat-trick yake ya pili tangu alivyowasili klabuni hapo akitokea AS Roma. Mchezaji wa mwisho kufunga hat-trick kabla ya Salah ni Luis Suarez.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.