Kimataifa

‘Msala’ wa Kodi Kumkimbiza Ronaldo Hispania

on

MADRID, Hispania
SAKATA la ulaghai wakati wa ulipaji ushuru linalomkabili mshambuliaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo huenda likamsababisha kuihama klabu hiyo kutokana na kuumizwa na suala hilo.

Waendesha mashtaka nchini
Hispania wanamtuhumu Ronaldo, 32, kwa kutumia ulaghai kutolipa mamilioni ya ushuru.

Ronaldo amekanusha tuhuma hizo na kusema kuwa amekuwa mkweli katika masuala ya kodi ambapo kwa sasa anafikiria kuondoka kabisa nchini Hispania.

“Anahisi kwamba amekuwa mkweli, ana sifa nzuri na alifanya kila kitu ipasavyo,” alisema mtu wa karibu wa nyota huyo.

Mkataba wa Ronaldo katika klabu hiyo una kifungu kinachoeleza kuwa ili mchezaji huyo aruhusiwe kuondoka, klabu inayomhitaji italazimika kugharamia kiasi cha paundi bilioni moja na hii ni kwa mujibu wa wakala wake Jorge Mendez.

“Amehuzunika sana na ameudhika kwa kweli. Hataki kukaa tena Hhispania kwa sasa anataka kuondoka.”

Ronaldo, aliyejiunga na Real Madrid akitokea Manchester United mwaka 2009 kwa ada ya pauni 80 milioni ambapo alisaini mkataba mpya wa miaka mitano na miamba hiyo Novemba 2016.

Mreno huyo anaweza kwenda China lakini washauri wake wangependa aendelee kucheza soka barani Ulaya pengine ahamie PSG au arejee nchini Uingereza.

Ronaldo aliyewasaidia Real kutwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya mara tatu na La Liga mara mbili, anatuhumiwa kulaghai maafisa wa Serikali ushuru wa takriban euro 14.7 milioni kati ya 2011 na 2014.

Real Madrid imetoa taarifa wakisema wana imani na mchezaji wao na kwamba wana uhakika atathibitisha kwamba hana makosa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *