Kitaifa

Msomi kumrithi Kahemele Simba

on

MBADALA wa Patrick Kahemele katika nafasi ya Katibu mkuu wa klabu ya Simba ni Dk. Arnold Kashembe ambaye ametajwa leo na uteuzi wake umeanza mara moja.

Jana kamati ya Utendaji ya klabu ya Simba ilikutana katika Hotel ya Serena, Dar es Salaam na kumteua Dk. Arnold kuchukua nafasi ya Kahemele aliyedumu kwa muda mfupi kabla ya kujiunga na kampuni ya Azam media.

Nafasi hiyo muhimu ya shughuli za kila siku za klabu ilikuwa wazi kwa miezi sita kabla ya Dk. Arnold ambaye ni msomi mwenye shahada ya uzamivu huku akiwahi kuwa mhadhiri katika vyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi kuchukua nafasi hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Idara ya Habari na mawasiliano huku pia ikiarifu kuwa Agosti 13 kutafanyika mkutano mkuu wa kawaida na wiki moja baadae kutafanyika mkutano mkuu ambao miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa itakuwa ni mabadiliko ya katiba.

Hii inatokana na matakwa ya katiba ya klabu hiyo ambayo inawataka kutoa notisi ya siku 30 kwa wanachama kabla ya kufanyika kwa mikutano yenyewe.

Aidha klabu hiyo itatoa taarifa zaidi juu ya maandalizi na taratibu za mikutano hiyo katika siku chache zijazo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *