Kitaifa

Msuva Aipeleka Stars Robo Fainali COSAFA

on

RUSTENBURG, Afrika Kusini
BAO la kusawazisha la dakika ya 68 lililofungwa na winga Simon Msuva limetosha kuipeleka Taifa Stars robo fainali ya michuano ya COSAFA licha ya kulazimishwa sare ya bao moja na Mauritius.

Stars sasa itacheza na wenyeji Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali siku ya Jumapili baada ya kumaliza kinara wa kundi A ikiwa na pointi tano sawa na Angola lakini ikiwazidi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Timu hizo zilienda mapumziko bila kufungana ambapo Mauritius walitangulia kupata bao kupitia kwa Joseph Stephen dakika ya 67 kabla ya Msuva kusawazisha dakika moja baadae na kuivusha Stars katika hatua hiyo.

Tanzania ni timu mwalika katika michuano hiyo kutokana na kutokuwa mwanachama wa Baraza la Michezo Kusini mwa Afrika (COSAFA).

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *