The sports Hub

Msuva aitabiria makubwa Serengeti Boys

0 11

LICHA ya kupoteza mchezo wa kwanza wa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa kufungwa mabao 5-4 dhidi ya Nigeria, winga Simon Msuva amesema  wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ wana nafasi ya kufanya vyema katika michuano hiyo.

Msuva anayecheza soka la kulipwa katika timu ya Difaa El Jadid nchini Morocco amedai ana imani kubwa na vijana hao kufanya  vyema lakini jambo la muhimu wanatakiwa kupambana vilivyo ili kuweza kushinda mechi  zilizobaki ikiwemo ya Angola kabla ya kumaliza na Uganda Aprili 20.

 “Binafsi naamini kuwa watafanya jambo kubwa sana ila wao wenyewe wanatakiwa kuipambania nchi yao. Pia jambo lingine la msingi ni kuhakikisha vijana wanarejea kwa haraka katika hali zao,” alisema Msuva.

Aliongeza kwa kuwataka wachezaji wa Serengeti Boys kusahau yaliyopita na kuangalia mchezo unaofuata kwa kuwa si wakati mwafaka wa kuendelea kujitafakari sababu zilizopelekea kupoteza mchezo huo.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.