Kitaifa

Msuva ataja siri ya mafanikio yake Yanga

on

WINGA Simon Msuva amebainisha kuwa mafanikio yake yaliyopelekea kujiunga na timu ya El Jadidi ya Morocco yanatokana mchango mkubwa wa wachezaji wenzake wa timu ya Yanga waliompa kwa kipindi chote alichokuwa nao.

Mchezaji huyo wa zamani wa Moro United amesema alipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki wa Yanga ambao umechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo.

Msuva amekuwa katika kiwango bora ambapo ameisaidia Yanga kutwaa mataji matatu ya ligi mfufulizo huku akiibuka mfungaji bora mara mbili kati ya misimu hiyo.

Nyota huyo anatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea Morocco akiwa na wakala wake Dkt. Jonas Tiboroha kwa ajili kukamilisha uhamisho likiwemo suala la kupima afya kabla ya kusaini mkataba kuwatumikia Al Jadida.

Simon Msuva akiwaanga wachezaji wenzake wa Yanga katika mazoezi ya leo asubuhi

Winga huyo aliwatembelea wachezaji wenzake wa Yanga katika mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru ili kuwaaga na kukiri mchango mkubwa waliompa katika mafanikio yake.

“Nilienda kuwaaga wachezaji wenzangu mazoezini leo, wamenisaidia sana kufika hapa nilipo sasa nawatakia kila la kheri kufanya vizuri katika michuano mbalimbali msimu ujao.

“Pia nawaomba Watanzania wenzangu kuniombea huko niendako kwakua mafanikio yangu ni faida kwa timu ya Taifa,” alisema Msuva.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *