Afrika

MSUVA: Messi kanipa maujanja yote

on

WINGA wa zamani wa Yanga, Simon Msuva aliyejiunga na timu ya Difaa El Jadidi ya Morocco amebainisha kuwa amepewa ‘maujanja’ na Ramadhan Singano ‘Messi’ juu ya maisha ndani ya klabu hiyo.

Singano ndiye wa kwanza kutua katika klabu hiyo akifanya majaribio ambapo mpaka sasa amefikisha wiki mbili na endapo atafanikiwa kufuzu ataungana na Msuva kwenye safu ya ushambuliaji.

Msuva ameiambia BOIPLUS kuwa jana alikutana na Singano na kuongea nae mambo mengi kuhusu timu hiyo jinsi gani anatakiwa kuishi ili kwenda nao sawa kutokana na utamaduni wao.

“Nimekutana na Singano, amenielekeza mambo mengi ambayo yamenipa mwanga jinsi ya kuishi katika timu yangu hii mpya. Kiukweli amenipa mwanga na kujua natakiwa nianzie wapi ili kufanikiwa hapa,” alisema Msuva.

Winga huyo amewaomba Watanzania wamuombee Singano ili afuzu majaribio yake ndani ya klabu hiyo wawe wawili na kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania.

Msuva alisema usiku wa leo timu yake itacheza mchezo wa kirafiki katika mji wa Casablanca na timu ambayo bado hajaijua jina lake.

“Tuna mchezo wa kirafiki leo jioni huko nyumbani itakuwa ni usiku katika mji wa Casablanca, natumai naweza nikawemo katika mchezo huo,” alisema Msuva.

Juzi Msuva alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *