Kitaifa

Mtibwa Yavunja ‘Ndoa’ na Nyota Saba na Kuanza Usajili

on

NYOTA saba wa timu ya Mtibwa Sugar wameachana rasmi na klabu hiyo baada ya mikataba yao kumalizika huku uongozi wa klabu hiyo ukitangaza kupata saini ya wachezaji wawili kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi.

Wachezaji ambao Mtibwa imeamua kutowaongezea mikataba ni Said Bahanuzi, Ally Shomari, Jaffary Salum, Vincent Barnabas, Ally Lundenga, Said Mkopi na Maulid Gole ‘Adebayor’.

Tayari wachezaji watatu kati ya hao wamesajiliwa na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu ambapo Shomari alikuwa wa kwanza kujiunga na Simba mapema mwezi huu.

Jaffary amejiunga na Kagera Sugar wakati Lundenga akisajiliwa na Mbeya City huku mkongwe Vincent Barnabas akitarajiwa kujiunga na benchi la ufundi la klabu hiyo ili kupata uzoefu japokuwa bado hajathibitisha.

Taarifa hiyo imetolewa kupitia mtandao rasmi wa klabu hiyo ambapo uongozi umejipanga kufanya usajili makini wa wachezaji wa kuziba mapengo hayo huku wakitarajia pia kupandisha nyota wengine kutoka katika timu yao ya vijana.

Wachezaji waliosajiliwa na Wakata miwa hao ni mshambuliaji Salum Ramadhan ‘Chuji’ kutoka Polisi Morogoro na beki wa kati Hussein Idd aliyekuwa JKT Oljoro ya Arusha.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *