Kitaifa

MWAMBELEKO: Simba Daraja tu, Safari Yangu Bado Sana

on

BEKI mpya wa klabu ya Simba Jamal Mwambeleko amesema kuwa anaitumia timu hiyo kama daraja kwa ajili ya kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Mwambeleko ambaye amejiunga na Simba akitokea Mbao FC ameiambia BOIPLUS kuwa malengo yake makubwa ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kukubali kutua kwa Wekundu hao.

Simba ni mabingwa wa kombe la FA ambapo imefuzu kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani kitu ambacho Mwambeleko anaamini kitaweza kumsaidia kutimiza malengo yake.

“Simba napita tu. Malengo yangu makubwa ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na hapa nilipo ni mahali sahihi kwangu kutimiza malengo yangu,” alisema Mwambeleko.

Mohamed Hussein ‘Tshabalala’

Akizungumzia nafasi yake ndani ya kikosi cha Simba Mwambeleko ambaye anacheza beki wa kushoto sawa na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliyecheza mechi zote msimu uliopita alisema atapambana kuhakikisha anamshawishi kocha Joseph Omog ampe nafasi ya kucheza.

“Mimi ni mchezaji ninayejitambua nafahamu Simba ni timu kubwa na kazi yangu ni soka kwahiyo nimejipanga kuhakikisha najituma mazoezini ili kumshawishi kocha anipe nafasi,” alisema Mwambeleko.

Mwambeleko ameungana na nyota wengine wapya kama Aishi Manula, Yusuph Mlipili, Shomari Kapombe na John Bocco ‘Adebayor’ waliojiunga na Simba kwa ajili ya msimu mpya wa ligi unaotarajiwa kuanza mwezi wa Agosti.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *