Kitaifa

Mwanjali akabidhiwa kitambaa cha unahodha Simba

on

METHOD Mwanjali ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa klabu ya Simba kuanzia msimu wa 2017/18 akichukua nafasi ya Jonas Mkude ambaye anakuwa mchezaji wa kawaida.

Mkude amedumu katika nafasi ya unahodha kwa mwaka mmoja alipochukua nafasi ya Mussa Mgosi aliyebadilishiwa majukumu na kuwa Meneja wa timu akifanikiwa kutwaa taji moja la kombe la FA msimu uliopita chini ya uongozi wake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya Habari na msemaji wa klabu hiyo Hajji Manara inasema benchi la ufundi limemteua raia huyo wa Zimbabwe kuwa nahodha akisaidiwa na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na mshambuliaji mpya aliyesajiliwa msimu huu John Bocco ‘Adebayor’.

Nahodha aliyemaliza muda wake, Jonas Mkude

Taarifa hiyo imesema kuwa uongozi unashukuru na kuthamini mchango wa Mkude kwa muda wote alipokuwa nahodha ambapo sasa anakuwa mchezaji mwandamizi.

Kikosi cha Simba kipo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi ambapo kitarejea nchini Agosti 5 kujiandaa na mchezo dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda kwenye mchezo wa tamasha la Simba Day, Agosti 8.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *