Kimataifa

Nani Kakudanganya? Ozil, Sanchez Hawaendi Kokote

on

Klabu ya Arsenal inajiandaa kufanya jaribio la mwisho la kuwashawishi nyota wake wawili Mesut Ozil na Alexis Sunchez kusaini mikataba mipya ya kusalia na Washika Bunduki hao.

Leo bodi ya klabu hiyo itakutana kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali likiwemo suala la mustakabali wa kocha Arsene Wenger ambaye mkataba wake unamalizika pamoja na nyota hao.

Arsenal wapo tayari kuwalipa nyota hao paundi milioni 30 kwa mwaka kwa wote wawili.

 

EDERSON NA MAN CITY KUELEWEKA NDANI YA SAA 24 ZIJAZO

Mlinda mlango wa timu ya Benfica Ederson Moraes atakamilisha uhamisho wa pauni 35 milioni kujiunga na Manchester City ndani ya saa 24 zijazo.

Usajili huo unaifanya City kuwa tayari kusajili nyota wawili baada ya wiki iliyopita kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa AS Monaco Bernado Silva kwa ada ya pauni 45 milioni.

Kocha wa City Pep Guardiola amepanga kufanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi hicho baada ya kupewa pauni 300 milioni kwa ajili ya kufanya usajili.

 

MILAN KUWANYAKUA MORATA, BELOTTI KWA MKUPUO

Kocha wa AC Milan Vincenzo Montella amekiri kuwa kuna uwezekano wa kusajili washambuliaji Alvaro Morata na Andrea Belotti ili kuimarisha kikosi hicho.

Milan imepata mmiliki mpya ambaye anataka kurejesha makali ya timu hiyo yaliyopotea katika miaka ya karibuni.

Belotti anayechezea Torino ya Italia amegeuka lulu baada ya klabu kubwa barani Ulaya kumuhitaji huku Morata akishindwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Zinedine Zidane ndani ya Real Madrid ambapo ameonyesha dalili za kutimka klabuni hapo.

CHELSEA KUMNG’OA BOATENG BAYERN

Mabingwa wapya wa ligi kuu nchini Uingereza timu ya Chelsea wameulizia uwezekano wa kumsajili beki wa kati wa Bayern Munich Jarome Boateng msimu ujao.

Boateng amekuwa katika kiwango ubora ambapo uongozi wa Bayern umesema hauko tayari kukubali raia huyo wa Ujerumani kuondoka klabuni hapo.

Hata hivyo chaguo la kwanza la kocha Antonio Conte ni beki raia wa Uholanzi anayechezea Southampton Virgil van Dijk anayepatikana kwa ada ya pauni 50 milioni.

BEGOVIC AKIMBILIA BOURNEMOUTH

Mlinda mlango namba mbili wa Chelsea Asmir Begovic anatarajia kujiunga na AFC Bournemouth kwa ada ya pundi 15 milioni.

Begovic ameshindwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi hicho ambapo kocha Antonio Conte amekuwa akimuamini zaidi Thibaut Courtois.

Dili hilo linategemewa kukamilika siku chache zijazo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *