Kitaifa

Nchimbi: Sitashangilia nikiwafunga Mbeya City

on

Akram Msangi, Dar
MSHAMBULIAJI mpya wa Njombe Mji, Ditram Nchimbi ameweka wazi kuwa hatoshangilia atakapoifunga timu yake ya zamani ya Mbeya City kutokana na mashabiki wa timu hiyo kuwa na mapenzi makubwa juu yake.

Ditram ambaye alikuwa akitajwa kuwaniwa na Yanga ameamua kuondoka Mbeya City baada ya Njombe Mji kumpa donge nono kuliko Wagonga Nyundo hao wanaodaiwa kutaka kumpa Sh 13 milioni.

Nchimbi alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Njombe Mji ambayo imepanda daraja msimu huu ambapo anatarajia kuisaidia kufanya vizuri kutokana na uzoefu alionao.

Mshambuliaji huyo ameiambia BOIPLUS kuwa alikuwa akipewa ushirikiano mkubwa na mashabiki wa City kitu kilichomfanya kujituma zaidi uwanjani ili kuwaridhisha na kumwamini.

“Nawaomba msamaha mashabiki wa Mbeya city kwa kuondoka ila wakumbuke mpira ni kazi yangu na maslahi ndiyo yaliyoniondoa. Ikitokea nikaifunga City sitashangalia kutokana na heshima ya mashabiki walionionyesha,” alisema Nchimbi.

Nchimbi alisema alikuwa na mchango mkubwa kuisaidia kupanda daraja timu ya Majimaji misimu mitatu iliyopita kwa kufunga mabao 10 lakini hajawahi kupendwa na mashabiki wa ‘Wanalizombe’ hao kama ilivyokuwa City.

“Nilifunga mabao 10 nakuisaidia Majimaji kupanda daraja lakini sijawahi kupendwa na mashabiki kama City. Popote nitakapokuwa nitawakumbuka sana mashabiki wa Mbeya City,” alisema Nchimbi.

Nchimbi ana uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani kama winga zote au mshambuliaji wa pili kitu ambacho kitakuwa faida kwa Njombe Mji.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *