The sports Hub

Nduda Ajigamba Kurejesha Kiwango Chake

0 33

KIPA wa Simba anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Ndanda, Said Mohamed ‘Nduda,’ amesema sababu ya kutoka Msimbazi ni ufinyu wa nafasi
ya kucheza.

Mlinda Mlango huyo alisema, uwepo wa makipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na Aishi Manula ndani ya Simba ulisababisha akose namba, hivyo ikambidi atafute sehemu ya kucheza na ndipo akajiunga na Ndanda ili akuze kiwango chache.

“Mazingira ya hapa ni mazuri, siwezi kusema nimepata nafasi ya
kucheza moja kwa moja kwa sababu nimewakuta watu hapa,
kikubwa napambana ili kuwafiti,” alisema Nduda.

Nduda aliyesajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar, kabla ya kutolewa kwa mkopo, aliongeza kwamba wanapambana kuhakikisha timu hiyo ikimaliza ligi kuu ikiwa katika nafasi nzuri, pia anaamini timu yake hiyo mpya itamrejeshea heshima yake iliyopotea.

 

Get real time updates directly on you device, subscribe now.