Kitaifa

Nduda Atisha Stars Ikikamata Namba 3 COSAFA

on

RUSTENBURG, Afrika Kusini
MLINDA mlango Said Mohammed ‘Nduda’ ameibuka shujaa wa Taifa Stars ikiiua Lesotho kwa mikwaju ya penati 4-2 katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya COSAFA nchini Afrika Kusini.

Mchezo huo ulilazimika kwenda kwenye hatua ya penati baada ya kumalizika kwa sare ya bila kufungana katika muda wa kawaida baada ya Nduda kufanya kazi kubwa ya kuokoa michomo ya wachezaji wa Lesotho ambao muda mwingi waliliandama lango la Stars.

Mbali na Nduda kocha Salum Mayanga aliwaanzisha wachezaji wengine ambao hawakupata nafasi katika mechi za awali ambao ni Nurdin Chona, Salmin Hoza na Stamil Mbonde ambapo walicheza vizuri licha ya uzoefu kuwaangusha.

Lesotho walilishambulia zaidi lango la Stars hasa kipindi cha kwanza lakini safu ya ulinzi ambayo iliongozwa na Chona pamoja na Salim Mbonde ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Abdi Banda, ilikuwa imara kumlinda Nduda.

Penati za Stars zilifungwa na Himid Mao, Simon Msuva, Banda na Raphael Daud huku Shiza Kichuya akikosa mkwaju wake.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *