The sports Hub

‘Ndugu’ wa Drogba Watinga TFF Kuishtaki Singida United

0 176

KAMPUNI ya Sports Plus Management inayomsimamia nyota wa Singida United, Diaby Aamara imeiandikia barua TFF ikitaka iingilie kati suala la madai ya mchezaji huyo yanayofikia dola 7,000 (zaidi ya sh. 15 milioni) kabla hawajachukua hatua zaidi ikiwemo kulifikisha jambo hilo FIFA.

Taarifa kutoka chanzo chetu zinadai kuwa barua hiyo iliyoandikwa jana Disemba 5 na kusainiwa na wakala Diallo Mahamede Lamine mwenye leseni ya FIFA namba 07044A imewasili TFF saa 6 mchana wa leo.

Kampuni hiyo imelalamikia kutolipwa kwa mteja wao Diaby baki ya dola 5,000 pamoja na fedha ya malipo ya wakala dola 2,000 ambayo haikulipwa kabisa na kufanya jumla iwe dola 7,000.

Boiplus Media ilimtafuta Mkurugenzi wa Singida, Festo Sanga kutaka kujua kama wamepokea taarifa za barua hiyo kuhusu nyota wao anayetokea taifa moja na mkongwe Didier Drogba (Ivory Coast) lakini simu yake haikuwa hewani.

Hii hapa barua yenyewe;

Get real time updates directly on you device, subscribe now.