Kitaifa

‘Ndugu’ wa Niyonzima kutua Dar Agosti 7

on

TIMU ya Rayon Sports ya Rwanda anakotekea kiungo mpya wa Simba, Haruna Niyonzima, itawasili nchini Agosti 7 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba katika tamasha la ‘Simba Day’ litakalofanyika siku moja baadae kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Tamsha hilo hufanyika kila mwaka Agosti 8 ambapo timu ya Simba huzindua jezi mpya pamoja na kuwatambulisha wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya msimu husika.

Baada ya utambulisho huo hufuatiwa na mchezo wa kirafiki ambapo msimu huu watacheza na mabingwa hao wa Rwanda timu ya Rayon.

Mkurugenzi wa kampuni ya EAG, Iman Kajura ambao ndio waratibu wa shughuli mbalimbali za masoko ya klabu hiyo, amesema tamasha hilo hutanguliwa na wiki ya Simba ambayo itaanza kesho ikiambata na mambo kadhaa ikiwemo kuwatembelea wachezaji wa zamani na kutoa msaada kwa watoto yatima.

Imani Kajura akizungumza na waandishi wa habari

“Tamasha la Simba Day hufanyika kila mwaka Agosti 8 ambapo wiki yake itaanza kesho kwa kutembelea matawi ya wanachama wetu, keshokutwa tutawatembelea wachezaji wetu wa zamani,” alisema Kajura.

Mbali na mchezo huo pia kutakuwa na mechi za utangulizi kati ya viongozi wa Simba na maveterani wa timu hiyo, pia vijana wa Simba na timu ya wanawake Simba Queens zitashuka dimbani siku hiyo.

Viingilio katika tamasha hilo vitatangazwa kesho ili mashabiki wanunue tiketi mapema kuepuka usumbufu siku ya tamasha.

Kikosi cha timu ya Simba kitarejea nchini Agosti 5 kikitokea Afrika Kusini kilipoweka kambi ya wiki tatu ya maandalizi ya ligi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *