Kimataifa

Neymar amaliza ziara ya United kiaina

on

MARYLAND, Marekani
MSHAMBULIAJI Neymar dos Santos Jr, amehitimisha ziara ya Manchester United nchini Marekani kwa kipigo kufuatia kuifungia Barcelona bao pekee katika mchezo wa kirafiki uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa FedEx Field.

Neymar ambaye anahusishwa na kutaka kujiunga na matajiri wa Ufaransa timu ya PSG kwa ada ya kufuru ya pauni 196 milioni alifunga bao dakika ya 31 baada ya kumzidi ujanja Antonio Valencia na kuhitimisha ziara ya Mashetani hao.

Raia huyo wa Brazil amekuwa kwenye ubora mkubwa ambapo wikiendi iliyopita alifunga mabao mawili, Barcelona ikiifunga Juventus mabao 2-0.

United haikuwa imepoteza mchezo wowote katika ziara hiyo baada ya kuzifunga timu za LA Galaxy, Real Salt Lake, Real Madrid na Manchester City nchini humo.

Kocha Jose Mourinho alifanya mabadiliko ya wachezaji nane katika kikosi kilichoshinda mikwaju ya penati dhidi ya Madrid wikiendi iliyopita.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *