Kitaifa

Niyonzima rasmi Simba, kutua wikiendi hii

on

KLABU ya Simba imetangaza rasmi kumalizana na kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima ambaye anatarajia kutua nchini wikiendi ijayo tayari kuwatumikia Wekundu hao.

Mkataba wa Niyonzima na timu yake ya zamani ya Yanga umemalizika mwezi uliopita na kuamua kujiunga na mabingwa hao wa kombe la FA akisaini mkataba wa miaka miwili.

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewaambia Waandishi wa Habari kuwa tayari wameshamalizana na kiungo huyo na kwa sasa ni rasmi Niyonzima ni mali yao.

Haji Manara, msemaji Simba SC

“Sio tetesi tena kwa sasa ni rasmi Niyonzima ni mchezaji halali wa timu ya Simba, kuna mambo anamalizia nchini Rwanda lakini wikiendi ijayo atatua nchini na kwenye tamasha la Simba Day atakuwepo,” alisema Manara.

Manara ametolea ufafanuzi pia suala la beki wao Juuko Murshid kutaka kusajiliwa na timu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini kuwa dili hilo halijafanyika na Mganda huyo bado ni mali ya Simba atakuwepo na Wekundu hao msimu ujao.

“Juuko ni mchezaji wetu bado ana mkataba, hakuna timu yoyote iliyoleta ofa juu yake. Kama hao Pirates wanamtaka waje mezani tuzungumze wala hatutamzuia kuondoka kikubwa ni makubaliano,” alisema Manara.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *