Kitaifa

NJOMBE MJI: Ditram Nchimbi mwanzo tu, mastaa kibao wanakuja

on

 

BAADA ya kuwajumuisha kikosini vijana kadhaa wapya wasio na majina makubwa, timu ya Njombe Mji imeanza kukusanya nyota wenye uzoefu na usiku wa leo wamemalizana na straika wa Mbeya City, Ditram Nchimbi.

Nchimbi alikuwa mhimili mkuu kwenye safu ya ushambuliaji ya City na sasa amesaini mkataba wa miaka miwili na wageni hao wa ligi kuu.

Afsa habari wa timu hiyo Solanus Mhagama ameithibitishia BOIPLUS juu ya usajili huo huku akisema mastaa kibao watatua klabuni hapo hivi karibuni.

Jezi mpya zaNjombe Mji

“Ni kweli Ditram (Nchimbi) amesaini mkataba wa miaka miwili muda mfupi uliopita, kwahiyo msimu ujao tutakuwa nae Njombe Mji.

“Ila huu ni mwanzo tu, kuna nyota wazoefu wengi tu watasaini hivi karibuni, subirini tutawajulisha,” alisema Mhagama.

Njombe iliyozindua jezi zake mpya hapo jana, imepanda daraja msimu huu pamoja na Singida United ya Singida na Lipuli ya Iringa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *