Kitaifa

Nyamlani Ajitoa Urais TFF

on

ALIYEWAHI kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani amejiengua kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Urais wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mkoani Dodoma.

Nyamlani amewasilisha barua ya kujiengua katika ofisi za TFF leo ikiwa ni siku moja tangu Kamati ya Uchaguzi ipitishe jina lake kuwa miongoni mwa wagombea 10 wanaowania nafasi hiyo huku akisema sababu ya kujitoa kwake ni masuala binafsi.

Hii ina maana kuwa wagombea wanaobaki kwenye kinyang’anyiro na kuhitajika kufika kwenye usaili kuanzia Juni 29, mwaka huu ni tisa wakiongozwa na Rais anayemaliza muda wake Jamal Malinzi.

Mbali ya Malinzi wengine wanaowania nafasi hiyo ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.

Waliojitokeza kuwania umakamu wa Rais na kurejesha fomu ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.

Mgombea Abdallah Mussa aliyekuwa akiwania nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji TFF kutoka Kanda Na. 1 (Mikoa ya Kagera na Geita) aliondolewa kwa sababu ya kutoambatanisha kivuli cha cheti cha elimu ya sekondari.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *