Kitaifa

Nyie wachukueni tu, Mtibwa wanaendelea kuziba mapengo

on

TIMU ya Mtibwa Sugar imeendelea kuziba mashimo yaliyoachwa na nyota wao waliotimka baada ya kufanikiwa kupata saini ya kiungo Hassan Dilunga kutoka Maafande wa JKT Ruvu.

Mtibwa imekuwa mhanga wa kuondokewa na nyota wake kila msimu mpya wa ligi unapoanza huku ikifanywa shamba la kuzalisha wachezaji wa kwenda kusaidia timu nyingine.

Wakata miwa hao tayari msimu huu imewapoteza mlinda mlango wake Said Mohammed ‘Nduda’, mabeki Salim Mbonde na Ally Shomari ambao wote wamejiunga na timu ya Simba.

Dilunga ambaye aliwahi kuitumikia timu ya Yanga amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuwatumikia wakali hao wa Turiani mkoani Morogoro kwa ajili ya msimu mpya wa ligi 2017/18.

Kiungo huyo alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Maafande wa JKT Ruvu msimu uliopita lakini ameshindwa kuinusuru kushuka daraja.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *