Kitaifa

Nyoso aibeba Misosi kutinga robo fainali Ndondo Cup

on

BEKI wa Kagera Sugar Juma Nyoso ameiongoza timu yake ya mtaani Misosi FC kutinga robo fainali ya michuano ya Ndondo Cup kwa kuifunga Faru Jeuri bao moja kwenye uwanja Kinesi.

Nyoso alichaguliwa mchezaji bora wa mchezo huo ambapo amekabidhiwa shilingi 50,000 kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo baada ya kuonyesha soka safi la kuvutia.

Kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ wa Faru alishindwa kuendelea na mchezo huo baada ya kuumia mguu dakika ya 45 baada ya kufanya kazi kubwa uwanjani.

Kiungo Laurent Mugia aliipatia Misosi bao hilo pekee dakika ya 68 kwa mpira wa adhabu nje ya 18 baada ya wachezaji wa Faru kufanya madhambi.

Faru ambayo iliongozwa na wakongwe kama Said Morad, Athuman Idd ‘Chuji’ na nahodha Edward Charles ilishindwa kuepuka kipigo hicho licha ya washambuliaji wao waliongozwa na kinda Cliff Buyoya kuonyesha soka safi na mashambulizi ya mara kwa mara.

Beki wa Misosi, Said Siwa alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika 87 kufuatia mchezo usio wakiungwana wakati wakishambulia lango la Faru.

Kesho Kauzu watacheza na Stimutosha katika mchezo wa hatua ya 16 katika uwanja huo huo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *