The sports Hub

Nyota Liverpool Apewa Mkataba Mpya Akiwa ‘Hospitali’

0 50

SIKU chache tu baada ya Joe Gomez kupata majeraha yatakayomfanya akae nje kwa wiki sita, klabu ya Liverpool imemuongezea nyota huyo mkataba wa miaka mitano na nusu itakayomweka Anfield hadi Juni 2024.

Gomez ambaye alisajiliwa na Liverpool kutoka Charlton Athletic Juni 2015, amefanyiwa maboresho makubwa katika vipengele vya mkataba wake mpya kutokaka na kiwango bora alichoonesha msimu huu na suala la yeye kuwa anaendelea na matibabu halikuwazuia majogoo hao kumpa dili mpya.

Baada ya kusaini mkataba huo Gomez hakuweza kuificha furaha yake akisema jambo hilo lina maana kubwa sana kwake.

“Nina furaha ya kuwa hapa, kucheza pamoja na kujifunza chini ya klabu mahiri pia kocha mahiri, sasa klabu inapoelekea inafurahisha na kutia moyo zaidi kutaka kujua yajayo juu ya timu ndio maana nipo hapa na nina furaha kubwa kuendelea kuwepo hapa,“ alisema Gomez.

Mlinzi huyo wa timu ya Taifa ya Uingereza alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Burnley katika mchezo ambao timu yake ilipata ushindi wa mabao 3-1.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.