Kitaifa

+VIDEO: Nyota Stars Wazidi Kutisha Sauzi

on

RUSTENBURG, Afrika Kusini
KIUNGO Mzamiru Yassin amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi kati ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Angola katika mechi iliyo malizika kwa sare ya bila kufungana kwenye michuano ya COSAFA inayofanyika nchini Afrika Kusini.

Hii ni mara ya pili kwa mchezaji wa Tanzania kupata tuzo ya mchezaji bora wa mechi baada ya Shiza Kichuya kuchaguliwa katika mechi dhidi ya Malawi juzi ambapo alifunga mabao mawili.

Katika mchezo huo Stars ilizidiwa umiliki mpira kwa muda wote ambapo mlinda mlango Aishi Manula alifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo ya washambuliaji wa Angola huku wao wakiwa hawajapiga hata shuti moja lililolenga lango.

Shiza Kichuya9

Sare hiyo imeifanya Stars kuendelea kubaki kileleni mwa kundi A ikiwa na pointi nne sawa na Angola wakiwazidi kwa tofauti mabao ya kufunga na kufungwa.

Timu za Malawi na Mauritius zina pointi moja kila moja kufuatia sare ya bila kufungana katika mchezo wa awali wa kundi hilo.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *