Kitaifa

Nyota Yanga waibukia Lipuli

on

BAADA ya kutoonekana uwanjani kwa muda mrefu hatimaye mshambuliaji wa Yanga Malimi Busungu na kiungo wa zamani wa mabingwa hao Omega Seme wamejiunga na timu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa kwa mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja.

Busungu ambaye aliwika na timu ya Mgambo JKT ya jijini Tanga kabla ya kusajiliwa na mabingwa hao miaka miwili iliyopita ameshindwa kujihakikishia kupata namba kwenye kikosi cha kwanza huku akiandamwa na mambo ya nje ya uwanja.

Omega tangu alipoondoka kwa mabingwa hao miaka kadhaa iliyopita ameshindwa kung’ara katika timu zinazoshiriki ligi kuu hivyo ataanza kuonekana kwa ‘Wanapaluhengo’ msimu ujao.

Omega Seme

Lipuli ambayo imepanda ligi kuu msimu huu imeanza kusajili wachezaji wazoefu kwa ajili ya kuongeza nguvu kikosini ili kuendana na kashkashi za ligi msimu ujao.

Siku mbili zilizopita timu hiyo ilikamilisha usajili wa mabeki Asante Kwasi kutoka Mbao FC na Paul Ngalema aliyetokea Ndanda FC.

Lipuli itacheza na mabingwa watetezi wa ligi kuu timu ya Yanga katika mchezo wake wa kwanza wa ligi msimu ujao Agosti 27 kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *