Kitaifa

Okwi Atua Dar na Kugeuka Bubu

on

MSHAMBULIAJI Emmanuel Okwi raia wa Uganda amewasili nchini usiku huu na kupokelewa na Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Gofrey Nyange ‘Kaburu’ katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

Baada ya kutua uwanjani hapo si Okwi wala Kaburu ambaye aliongea chochote na Waandishi wa Habari waliokuwepo ambapo Kaburu ameahidi kuitisha mkutano wa Waandishi wa habari.

Juzi Alhamisi Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa klabu hiyo Zacharia Hanspope alisema mshambuliaji huyo kipenzi cha Wana Simba atawasili leo na ndicho kilichotokea.

Okwi anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia Wekundu hao kwa ajili ya mashindano mbalimbali kuanzia msimu ujao.

Simba itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani baada ya kutwaa taji la kombe la FA.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *