The sports Hub

PAWASA: uwezekano wa Tanzania kufuzu Afcon upo

0 24

Beki wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Boniface Pawasa amesema kikosi hicho kina uwezo wa kuifunga Uganda na kucheza Fainali za Mataifa Afrika (Afcon) kutokana na ubora wa wachezaji waliopo.

Stars inatarajia kukutana na Uganda Jumapili katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo katika msimamo wa kundi L, Uganda tayari imeshakata tiketi ya kucheza Afcon baada ya kufikisha pointi 13, Taifa Stars inashika nafasi ya pili na pointi tano sawa na Lesotho huku Cape Verde ikiwa na pointi nne.

“Kwa kikosi ninachokiona uwezekano wa Tanzania kufuzu Afcon upo licha ya kuwa kundi kukaa ibaya kwa sababu hatujajua wenzetu nao watafanya nini ila kwa kuifunga Uganda, Taifa Stars inaweza,” alisema.

Mchezaji huyo alizidi kufafanua kutokana na msimamo wa kundi L, endapo wachezaji watajituma na maandalizi yakafanywa vizuri, Stars inaweza kuwafuta Watanzania machozi ya muda mrefu.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.