Kitaifa

PrincessBet Kurejesha Furaha kwa Yatima

on

KAMPUNI ya inayojihusisha na michezo ya kubatisha ya PrincessBet na Princess Cassino imewataka wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia watu wenye mahitaji maalum kwa ajili ya kurejesha kwa jamii kinachopatikana.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja mkuu wa kampuni hiyo David Kuff alipokuwa akizundua awamu ya pili ya marekebisho ya kituo cha Mwandaliwa Ophan Center kilichopo Mbweni ambapo watatoa mashuka, magodoro na vyandarua ili kurejesha furaha kwa watoto hao.

Akizungumza na wadau mbalimbali zikiwemo timu za mpira wa wavu ambazo zinashiriki ligi ya mkoa wa Dar es Salaam na wadhamini, Kuff alisema wanataka kurejesha furaha katika kituo hicho ambacho kina watoto 94.

“Hii ni awamu ya pili, ya kwanza tuliwarekebishia jiko na awamu ya tatu itakuwa masula ya afya na elimu,” alisema Kuff.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama cha wavu Dar es Salaam (DAREVA) Yusuph Mkarambati ameishukuru kampuni hiyo kwa kujitolea kusaidia kituo hicho ambapo ameyataka makampuni na watu binafsi kujitoa kusaidia watu wenye mahitaji maalum.

Akitoa neno la shukrani kwa kampuni hiyo kwa niaba ya kituo cha Mwandaliwa mmoja wa watoto hao Hussein Athuman ameishukuru PrincessBet kwa msaada huo kutokana na changamoto wanazokutana nazo huku akisisitiza wadau wengine waendelee kujitokeza kwakua hawana udhamini.

Miongoni mwa timu za mpira wa wavu zilizokuwepo kwenye hafla hiyo ni CDS, JKT, DIT, Polisi Marine, Kigamboni, Tanzania Prisons, Makongo na Kinyerezi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *