Kimataifa

Rooney Kuandika Historia Taifa

on

MERSEYSIDE, Uingereza
KUFUATIA mfungaji bora wa muda wote wa Manchester United Wayne Rooney kurejea katika timu yake ya zamani ya Everton ‘Toffees’ baada ya miaka 13 kupita, kuna uwezekano straika huyo akaandika historia kwa kuichezea mechi ya kwanza ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Everton inatarajia kupambana na Gor Mahia Julai 13 na kwamba kukamilika kwa usajili huo ni dalili tosha kuwa mkali huyo wa mabao atatua Bongo na kukanyaga nyasi za dimba hilo la Taifa.

Rooney, 31, ameichezea United mechi 559 na kufunga mabao 253 ambayo hakuna mchezaji mwingine wa Mashetani hao Wekundu aliyefikia.

Rooney ameshinda mataji matano ya ligi kuu, moja klabu bingwa Ulaya, Kombe la Europa na FA tangu alipojiunga na United akitokea Toffees kwa ada ya pauni 27 milioni mwaka 2004.

Nahodha huyo wa timu ya Uingereza alisema ni furaha kwake kurejea katika timu iliyomlea ambapo amekiri itakuwa siku ya hisia kwake kucheza mechi ya kwanza akiwa na Everton.

“Ni hisia kubwa kurejea tena Everton. Itakuwa furaha kukutana na wachezaji wenzangu kwenye mazoezi na mechi pia.

Dili hilo na Rooney linakuja siku moja baada ya United kufanikiwa kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku kutoka Everton kwa ada ya pauni 75 milioni baada ya timu zote kukubaliana.

“Nimerejea Everton kwakuwa ndiyo timu ninayoishabikia, timu iliyonilea na ninaiona itakuwa na mafanikio katika siku za usoni,” alisema Rooney, ambaye aliifungia mabao 17 katika michezo 77 alipoitumikia miaka kadhaa iliyopita katika uwanja wa Goodison.

“Napenda kuwa sehemu ya mafanikio hayo. Najua itakuwa presha kwangu kucheza kwa kiwango bora lakini naamini naweza kuisaidia timu hii uwanjani kusonga mbele.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *