Kitaifa

Ruvu Shooting Yapiga Chini Nyota 10

on

UONGOZI wa Maafande wa Ruvu Shooting umetangaza kuachana na wachezaji 10 lakini imewataja sita na wanne watatajwa siku chache zijazo kutokana na sababu mbalimbali.

Wachezaji hao wametemwa kutokana na taarifa ya kocha Malale Hamsini aliyotuma kwa uongozi kuwa hatoendelea nao kwa msimu mpya wa ligi 2017/18.

Ofisa Habari wa Maafande hao Masau Bwire amewataja wachezaji hao kuwa ni Elius Emmanuel ambaye alicheza mechi moja msimu mzima, Ismail Mgunda aliyetoroka kambini na mpaka sasa hajulikani alipo na Richard Peter ambaye hakucheza mechi hata mmoja msimu mzima.

Wengine walioachwa ni Claide Luita ambaye alicheza michezo mitatu mzunguko wa kwanza wa pili hakucheza akaamua kuondoka mwenyewe ingawa kocha Malale alimsifia kwa kipaji na ubora wake, Amour Bakari aliyecheza mchezo mmoja tu kutokana na uwezo mdogo na maumivu ya mara kwa mara na Alex Sety ambaye alicheza michezo sita.

“Uongozi wa Ruvu Shooting ulikutana jana chini ya Mwenyekiti wake Kanali Charles Mbuge na kufikia makubaliano ya kuwaacha nyota 10 na tayari tumewatangaza sita wengine wanne watatajwa siku chache zijazo,” alisema Masau.

Katika kikao hicho pia wamekubaliana kusajili wachezaji tisa katika nafasi za beki wa kati mmoja, viungo wa pembeni wawili, viungo wakabaji wawili, beki wa kulia mmoja na washambuliaji watatu.

Masau alisema pia Uongozi umeunda timu ya watu wanne kwa ajili ya kufanya usajili kwa uangalifu na usiri mkubwa ili kukiandaa kikosi chao kwa msimu mpya wa ligi utakaonza mwezi Agosti.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *