Kitaifa

Saa Chache Kabla Dirisha Kufunguliwa, Njombe Mji Waweka Mipango Hadharani

on

ZIKIWA zimesali saa chache dirisha la usajili lifunguliwe rasmi timu ya Njombe Mji imejipanga kusajili wachezaji vijana watakaoleta changamoto kwenye ligi msimu ujao.

Kauli hiyo imetolewa na kocha wao mkuu Hassan Banyai ambaye amesema hawakupanda ligi kuu kwa bahati mbaya na wamejipanga kufanya makubwa kwenye ligi hiyo ikiwemo suala la kunyakua ubingwa.

Banyai ameiambia BOIPLUS kuwa tayari wameshafanya usajili kwa baadhi ya nyota ambao amegoma kuwataja hadi dirisha litakapofunguliwa usiku huu huku akijinadi kuwa utakuwa usajili mzuri ambao umeendana na mahitaji ya timu.

“Tumesajili wachezaji kadhaa lakini siwezi kukutajia kwa sasa kwakua dirisha halijafunguliwa. Wachezaji wengi tutakaowatumia ni vijana zaidi na wazoefu watakuwa wachache kikosini,” alisema Banyai.

Kikosi cha Njombe Mji

Banyai aliongeza kuwa wataingia kambini Jumatatu ijayo kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi unaotarajiwa kuanza mwezi Agosti ambapo alisema watu wasiwachukulie kawaida kwani wamejipanga kufanya mapinduzi kwenye soka na uwezo huo wanao.

“Tumekuja kufanya mapinduzi ya soka, hatukuja kushiriki bali kushindana kwahiyo wasituchukulie poa tunaweza kuwashangaza msimu huu,” alisema Banyai.

Njombe Mji imeungana na timu za Singida United na Lipuli zilizopanda  daraja msimu huu baada ya JKT Ruvu, African Lyon na Toto Africa kushuka daraja.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *