Kitaifa

Salmin Hoza Sasa Rasmi Azam

on

AZAM FC imemalizana na mshambuliaji Salmin Hoza aliyekuwa akiichezea Mbao FC ambapo wamempa mkataba wa miaka miwili atakaoanza kuutumikia msimu ujao wa ligi.

Huu ni usajili wa tatu kwa Azam kuufanya ambapo walianza na Waziri Junior kutoka Toto African na Mbaraka Yusuph aliyekuwa akiichezea Kagera Sugar ambao wote walikuwa wakiwaniwa na Yanga.

Yanga ilishindwa kuwanasa wachezaji hao kutokana na sababu inayoelezwa kuwa ni ukata unaowakabili japokuwa walifanya mazungumzo ya awali na wachezaji hao.

Salmin Hoza kushoto akiambana na Ibrahim Ajib wa Simba

Azam wao walimfuata Hoza jana Ijumaa jijini Mwanza baada ya Yanga kutangulia na kumpa Sh 5 milioni ili asisaini timu nyingine lakini Azam wao wamekwenda na pesa taslimu na kumalizana naye jana usiku.

Habari za ndani zinasema kuwa wachezaji hao wawili watatambulishwa muda wowote kuanzia kesho Jumapili.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *