Kitaifa

Samatta aibukia Mbeya City

on

BAADA ya kuachana na Maafande wa Tanzania Prisons kiungo Mohammed Samatta amejiunga na majirani zao Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

Samatta ni miongoni mwa wachezaji ambao hawakuwa askari na kutokana na sheria mpya za jeshi la Magereza kupunguza idadi ya watu wasio wanajeshi ndani ya kikosi hicho, kiungo ameamua kujiunga na Wagonga nyundo hao.

Baada ya kusaini mkataba huo Samatta amesema alikuwa akitamani kujiunga na timu hiyo kutokana na umakini wa uendeshwaji wake hivyo ameona ni sehemu salama kwake katika soka.

“Mara zote nikiwa Mbeya nikichezea Prisons tunapopishana na wachezaji wa City barabarani au kucheza nao uwanjani nimekua na shauku kubwa ya kutaka kucheza soka nikiwa na jezi ya zambarau na kuwa sehemu ya klabu hii,” alisema Samatta.

Mbeya City wanaendelea kuimarisha kikosi chao kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi ambapo tayari wamesajili mshambuliaji Idd Seleman ‘Ronaldo’, beki Erick Kyaruzi huku ikimuongeza mkataba Haruna Shamte.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *