Kimataifa

SAMATTA: Huyo Sander ni wa Madrid sio Arsenal

on

“Huyo jamaa ni bonge la mchezaji” hiyo ni kauli ya straika wa KRC Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta akimzungumzia kinda Sander Berge anayekipiga naye klabuni hapo.

Berge anafukuziwa na Arsenal ya Uingereza kwa udi na uvumba baada ya maskauti wa ‘Washika Bunduki’ hao kujiridhisha juu ya uwezo wa kiungo huyo raia wa Norway aliyeonyesha kiwango kikubwa miezi michache tu tangu ajiunge na Genk.

Mbwana Samatta

“Niliwahi kumwambia Sander mwenyewe kuwa wewe ni mchezaji mkubwa unayestahili kucheza timu kubwa kama Real Madrid, Chelsea na nyinginezo.

“Ana uwezo mkubwa sana, kama Arsenal watamchukua basi hapo atapita tu aende zake Madrid huko,” alisema Samatta ambaye amecheza naye kwa miezi sita tu klabuni hapo.

Arsenal wapo tayari kutoa kitita cha paundi 18 milioni kwa ajili ya kupata saini ya ‘mkata umeme’ huyo ambaye mkataba wake na Genk unaisha 2021.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *