Kitaifa

Sasa rasmi winga Msuva, winga Messi El Jadidi

on

WINGA wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na wababe wa Morocco Difaa El Jadidi inayoshiriki ligi kuu nchini humo huku akipokelewa na Ramadhan Singano ‘Messi’ aliyesajili hivi karibuni.

Msuva aliongozana na wakala wakeJonas Tiboroha kwenda nchini Morocco kukamilisha ‘deal’ hiyo inayomfanya winga huyo mwenye miaka 26 aanze maisha ya soka la kulipwa nje ya Tanzania kwa mara ya kwanza.

Ramadhan Singano ‘Messi’ akiitumikia El Jadidi

Baada ya kusaini mkataba huo Msuva alitambulishwa mbele ya wanahabari na sasa ataungana na Messi ambaye alimaliza mkataba wake na Azam FC kabla hajajiunga na waarabu hao.

Msuva alichelewa kwenda nchini Morocco kutokana na majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliyokuwa inachuana na Rwanda kutafuta tiketi ya kufuzu kwa michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *