Kitaifa

Serengeti Boys Kutua Nchini Kesho

on

TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ itawasili nchini kesho mchana ikitokea nchini Gabon baada ya kutolewa kwenye michuano ya vijana ya Afrika inayoendelea nchini humo.

Serengeti ilitolewa juzi na Niger baada ya kukubali kichapo cha bao moja na kumaliza nafasi ya tatu kwenye kundi B ikiwa na pointi nne sawa na Niger lakini wametolewa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Ofisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Alfred Lucas ambaye yupo pamoja na timu hiyo amesema wataondoka kesho Libraville saa 1:15 usiku ambapo watafika nchini saa 8:50 mchana na kuelekea kwenye hotel ya Urban Rose kwa ajili ya kambi.

“Timu itaingia nchini kesho kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini na itaelekea moja kwa moja kambini Urban Rose,” alisema Lucas.

Serengeti ilikuwa na matumaini makubwa ya kufuzu kucheza michuano ya dunia kwa vijana itakayofanyika mwezi Novemba nchini India kama ingeweza kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali lakini kipigo kutoka kwa Niger kilipoteza kabisa ndoto zote.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *