Kitaifa

Shaffih Dauda ataja kilichosababisha akamatwe

on

SIASA za Uchaguzi wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika mwezi ujao mkoani Dodoma zimetajwa kuwa ndio sababu ya viongozi 10 wa soka kushikiliwa na Taasisi ya Kuthibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza.

Usiku wa kuamkia jana viongozi hao wakiwemo Almas Kasongo, Shaffih Dauda, Elius Mwanjali, Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mwanza na wengineo walikamatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za kuanza kampeni kabla ya muda ikihususishwa na suala la rushwa pia.

Akizungumza katika kipindi cha Sports Extra ya Clouds FM jana usiku mmoja wa walioshikiliwa na TAKUKURU, Shaffih amesema walitegewa mtego wa kuwachafua ili waonekane hawafai kwenye kinyang’anyiro hicho japokuwa amesifu utendaji kazi wa taasisi hiyo wa kuzingatia weledi wa kazi zao.

“Tulikuwa tunakula chakula cha usiku Villa Park, mara wakaja watu wakatuuliza tulikuwa tunafanya nini wakatuchukua kutupeleka kuhojiwa, wakatupekua lakini hawajaona kitu chochote kibaya wakaja hadi hotelini ila hawajaona chochote.

“Ilitubidi tuwe wapole tusibishane na mamlaka za Serikali, lakini moja kwa moja hizi ni siasa za uchaguzi, kuna wagombea wanahofia uwepo wangu kwenye kinyang’anyiro, ila kutoka ndani ya moyo wangu nawapongeza TAKUKURU kwa jinsi wanavyofanya kazi zao kwa weledi mkubwa,” alisema Dauda.

Watuhumiwa wote wapo nje kwa dhamana huku uchunguzi dhidi yao ukiendelea na endapo watakutwa na hatia sheria itachukua mkondo wake ikiwemo suala la kufikishwa Mahakamani.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *