Kitaifa

Sheria mpya za Magereza zamkimbiza Samatta Prisons

on

JESHI la Magereza nchini limeanzisha sheria mpya michezo ambapo sasa litakuwa linawatumia wachezaji ambao ni waajiriwa wa jesho hilo tu na ndiyo maana wameshindwa kumpa mkataba mpya mshambuliaji wao Mohammed Samatta.

Samatta alisajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja na Prisons ambao umemalizika na sasa inadaiwa Mbeya City wamefanya naye mazungumzo na kilichobaki ni kumalizana kwenye mkataba.

Samatta sio askari Magereza na amekuwa miongoni mwa nyota ambao hawatakuwepo kwenye kikosi cha Prisons msimu ujao pamoja na wenzake watano akiwemo Andrew Antala na Victor Hangaya huku waliobaki ni raia wanne pekee.

Samatta ameiambia BOIPLUS kuwa kutokana na sheria ziliyowekwa na jeshi la Magereza msimu ujao hatokuwa na timu hiyo ambapo kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na Mbeya City kwa ajili ya kujiunga nao kama watafikia makubaliano.

“Sheria za Magereza zinataka kupunguza wachezaji ambao ni raia kwahiyo sitachezea Prisons msimu ujao.

“Viongozi wa Mbeya City wamenifuata wanahitaji huduma yangu, mazungumzo yanaenda vizuri tukifikia makubaliano nitajiunga nao,” alisema Samatta.

Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe alikiri kuwepo kwa mazungumzo na mshambuliaji huyo na kwamba bado wana nafasi ya kufanya usajili wao.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *