Kitaifa

Si mlizusha?, subirini kesho muione Simba

on

GAUTENG, Afrika Kusini
BAADA ya mazoezini ya wiki mbili kambini nchini Afrika Kusini na ‘uzushi’ wa Simba kupigwa 7-0 na Royal Eagles, hatimaye kocha Joseph Omog ‘atazitest’ silaha zake kesho katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa katika jiji la Johannesburg.

Mchezo huo utakuwa ni kwanza kwa Wekundu hao ambapo kocha Omog anatarajiwa kuwapanga nyota wake waliosajiliwa msimu huu akiwemo Emmanuel Okwi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na mawasiliano ya klabu hiyo, baada ya mchezo huo wa kesho Simba itashuka tena dimbani Alhamisi kucheza na Bidvest.

Mbali na Okwi wachezaji wapya wengine wa Simba wanaotarajiwa kuonekana kesho ni Said Mohammed ‘Nduda’, Salim Mbonde, Ally Shomari, Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko, Yusuph Mlipili na John Bocco.

Wakati huo huo mlinda mlango Aishi Manula anatarajia kujiunga na kikosi hicho kesho baada ya kukamilisha usajili kwa kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Azam FC.

Manula alishamalizana na wekundu hao mapema lakini walishindwa kutangaza kutokana na mchezaji kuwa ndani ya mkataba na Azam FC.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *