Kitaifa

Siku Ngumu kwa Vigogo wa Soka Nchini

on

LEO ni siku mbaya na ngumu sana kwa viongozi wa soka baada ya Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi na katibu mkuu wake Mwesigwa Celestine kurudishwa mahabusu hadi Julai 3 kutokana na kukosa dhamana katika tuhuma zinazo wakabili.

Hili lilitokea saa chache baada ya Rais wa Simba Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kupelekwa mahabusu hadi Julai 13 siku ambayo kesi yao ya matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji pesa itakaposomwa tena katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Malinzi na Mwesigwa walikamatwa usiku wa juzi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kushikiliwa kwa muda wote kabla ya kupandishwa Mahakamani leo ambapo watasubiri hadi Julai 3 kesi hiyo itakapotajwa tena.

Hii ina maana kuwa Malinzi hataweza kutetea nafasi yake ya Urais wa TFF kutokana na kushindwa kufanya usaili ulioanza leo na kumalizika Julai mosi siku ambayo atakuwa hajatoka mahabusu jambo litakalomfanya yeye na Kaburu waenguliwe kwenye kinyang’anyiro hicho kwa mujibu wa kanuni.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *