Kitaifa

Silaha saba zaongezwa Stars kuivaa Rwanda

on

NYOTA saba wameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mechi ya kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) dhidi ya Rwanda Jumamosi kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Nyota hao ambao hawakuwepo kwenye kikosi cha Stars kilichomaliza nafasi ya tatu katika mashindano ya COSAFA iliyomalizika jana nchini Afrika Kusini wameitwa kwa ajili ya kuongeza nguvu kuelekea mchezo huo muhimu.

Kocha wa timu hiyo Salum Mayanga amewataja wachezaji hao mbele ya waandishi wa Habari katika ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kuwa ni Said Ndemla (Simba) , Joseph Mahundi (Azam) ,Boniface Maganga (Mbao FC), Ramadhan Kabwili (Serengeti Boys), Athanas Mdamu (Alliance Academy) , John Bocco (Azam) na Kelvin Sabato (Majimaji) .

Mayanga alisema washambuliaji Thomas Ulimwengu na Elius Maguri hawakujumuishwa kutokana na kucheza soka la kulipwa nje ya nchi huku Mbaraka Yusuph, Shaban Idd na Beno Kakolanya wakiachwa sababu ya majeruhi.

“Tumeongeza wachezaji saba kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Rwanda wikiendi ijayo, ambao wataungana na wale tuliokuwa nao Afrika Kusini kwenye michuano ya COSAFA,” alisema Mayanga.

Kikosi cha Stars kinaondoka leo jioni kuelekea Mwanza kwa ajili ya kambi kabla ya mechi ya Jumamosi Julai 15.

Kikosi kamili kilichoitwa ni makipa Aishi Manula, Said Mohamed na Ramadhan Kabwili. Walinzi ni Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Boniface Maganga, Gadiel Michael, Salum Mbonde, Abdi Banda na Nurdin Chona.

Viungo ni Himid Mao, Salmin Hoza, Shiza Kichuya, Simon Msuva, Raphael Daud, Erasto Nyoni, Joseph Mahundi, na Said Ndemla.

Washambuliaji ni Kelvin Sabato, Stamil Mbonde, John Bocco, Athanas Mdamu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *