Kitaifa

Simba, Jang’ombe Boys ‘Dege’ Moja na Singida United

on

TIMU za Simba na Jang’ombe Boys zimeondolewa kwenye mashindano ya SportPesa Super Cup yanayoshirikisha timu kutoka Tanzania na Kenya. Mashindano hayo yanafanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga ndiyo timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye mashindano hayo huku Singida United ikiwa ya kwanza kufungasha virago hapo jana Jumatatu walipofungwa kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya AFC Leopard ya Kenya.

Yanga ambao wameingia nusu fainali watacheza na Leopard huku Nakuru All Stars wao wataingia dimbani kucheza na Gor Mahia ambayo imeifunga Jang’ombe Boys kwa bao 2-0, mechi ambayo ilikuwa ya kwanza kuchezwa leo Jumanne.

Beki mpya wa kushoto wa Simba, Jamal Mwambeleko (kulia) ‘akimfinya’ kiungo wa Nakuru, Sosi Dennis Nandwa

Jang’ombe ambayo ilikuwa inaongozwa na kiungo mkongwe Abdi Kassim ‘Babi’ ilicheza vizuri lakini maumbo makubwa ya wachezaji wa Gor Mahia yalikuwa kikwazo kutokana na Wanzibar hao kuwa na maumbo madogo.

Simba ambayo ilicheza mechi hiyo ya pili ilikuwa ikipewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo nayo imetolewa katika mchezo uliomalizika jioni ya leo na Nakuru All Stars kwa mikwaju ya penati 5-4.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufangana licha ya Simba kuonekana walikuwa na nafasi kubwa ya kumaliza mchezo huo mapema kutokana na kutengeneza nafasi nyingi lakini safu yao ya ushambuliaji ilikuwa butu.

Wachezaji wa Nakuru wakishangilia baada ya kufanikiwa kuitoa Simba

Wachezaji Javier Bokungu, Mwinyi Kazimoto, Hafidh na Feston Munezero walifunga penati kwa upande wa Simba wakati Daniel Agyei mkwaju wake ukiota mbawa.

Upande wa Nakuru penati zao zilifungwa na Baraka Jerome, Amani Kyata, Maina Geoffrey, Amakanji Ekuba na Daniel na kutinga hatua ya nusu fainali.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *