Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Simba Kucheza Nusu Fainali Bila Lechantre

0 4,632

HABARI ndio hiyo, yaliyokuwa yakisemwa sasa yametimia. Kuna kila dalili kuwa klabu ya Simba imeachana na kocha wao Pierre Lechantre na hatokuwepo kwenye mechi ya nusu fainali ya Sportpesa Super Cup mchana huu dhidi ya Kakamega Homeboys.

Wadau wa Simba wamekuwa wakipingana na mfumo wa kocha hiyo wakidai timu yao haichezi soka la kuvutia na sasa inaonyesha viongozi wameamua kumtimua huku Masoud Juma akikabidhiwa jahazi aliongoze hadi mwisho wa michuano hiyo.

Related Posts
1 of 32

Taarifa zinadai kocha hiyo ataondoka leo kurejea jijini Dar tayari kwa safari ya kuelekea nchini kwao. Kocha huyo ametimuliwa pamoja na kocha wa viungo Mohammed Aymen Hbibi raia wa Morocco.

Masoud Djuma akiongoza mazoezi ya Simba

Masoud ameonekana akiwaongoza wachezaji kupasha misuli kabla ya pambano hilo huku Lechantre na Hbibi wakiwa jukwaani.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...