Kitaifa

Simba Sasa ‘Yahamia’ Kagera

on

BEKI wa kati Hassan Isihaka amewaongoza wachezaji kadhaa waliowahi kuitumikia timu ya Simba kujiunga na Kagera Sugar kwa ajili ya msimu mpya wa ligi utakaonza mwezi Agosti.

Isihaka ambaye alikuwa anachezea African Lyon iliyoshuka daraja amejiunga na Kagera jana ambapo sasa ataungana na beki Juma Nyoso na Peter Mwalyanzi ambao nao wamejiunga na ‘Wana Nkurukumbi’ hao siku chache zilizopita.

Juma Nyoso

Nyota hao watatu wataungana na wengine wawili ambao nao waliwahi kuchezea Simba mlinda mlango Juma Kaseja na beki Mohammed Fakhi waliokuwepo klabuni hapo tangu msimu uliopita.

Nyoso alifungiwa miaka miwili kutojihusisha na soka kipindi akiichezea Mbeya City baada ya kumfanyia kitendo cha udhalilishaji mshambuliaji John Bocco wakati Mwalyanzi alitolewa kwa mkopo Lyon ili kupandisha kiwango chake.

Kupitia mtandao wa Instagram wa klabu hiyo, Kagera imethibitisha kuzinasa saini za nyota hao ambao kwa pamoja watakuwa na jukumu la kulinda heshima iliyongwa klabuni hapo msimu uliopita kwa kufanikiwa kukamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Peter Mwalyanzi

Kagera ambayo inanolewa na kocha Meck Mexime ilitisha nyuma ya Simba na Yanga kwenye msimamo wa ligi msimu uliopita na sasa imeamua kuhakikisha inapiga hatua zaidi kwa kusajili wachezaji wazuri ili kufanya vizuri zaidi msimu ujao.

Mbali na nyota hao Kagera wamekamilisha usajili ya wachezaji Ludovic Venance, Omari Daga, Abdallah Mguhi (Lyon), Japhary Salum Kibaya (Mtibwa Sugar), na Said Kipao (Ruvu Shooting).

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *