Kitaifa

Simba Waendelea Kuibomoa Mtibwa

on

BEKI wa kati Salim Mbonde wa Mtibwa Sugar ambaye yupo katika kiwango bora kwa sasa amejiunga na timu ya Simba mchana wa leo kwa mkataba wa miaka miwili na kuendeleza historia ya klabu hiyo kuvuna kutoka katika mashamba hayo ya miwa yaliyopo Manungu.

Mbonde ametua nchini usiku wa kuamkia leo akitokea Afrika Kusini alipokuwa na timu ya taifa iliyokuwa ikishiriki michuano ya COSAFA ambapo Tanzania imekamata nafasi ya tatu.

Mbonde alishirikiana na mabeki wengine wa kati Abdi Banda, Erasto Nyoni na Nurdin Chona kutengeneza safu imara ya ulinzi ya Stars ambapo nyota huyo ndio alikuwa kiongozi wao.

Simba imeamua kuendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa ligi baada ya kushindwa kuchukua ubingwa kwa miaka mitano ambapo mwakani wataiwakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mbonde anaungana na beki mwenzake Ally Shomari aliyejiunga na Simba akitokea Mtibwa hivi karibuni. Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin na Mohammed Ibrahim walijiunga na Simba wakitokea Mtibwa msimu uliopita.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *