Kitaifa

Simba Wamalizana na Mkude Anayesubiriwa Yanga

on

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kuzima jaribio la hatari baada ya kumsainisha mkataba mpya wa miaka miwili nahodha Jonas Mkude kufuatia aliyekuwa amekabilia kujiunga na watani wao wa jadi Yanga.

Mchana wa leo mtandao huu uliripoti taarifa ya nahodha huyo kutengewa dau nono mitaa ya Jangwani lakini jioni hii Viongozi wa Wekundu hao walifanikiwa kuzima jaribio hilo kitendo ambacho kitarejesha furaha kwa mashabiki wa Simba.

Mkude mwenyewe ameithibitishia BOIPLUS kuwa amesaini mkataba mpya na waajiri wake hao ambao wamemkuza toka akiwa kijana mdogo mpaka kufikia kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi hadi kuteuliwa kuwa nahodha.

Mkude alisema alikuwa anaipa Simba nafasi kubwa baada ya kumalizika kwa mkataba wake licha ya kupokea ofa kutoka katika timu mbalimbali ambazo zilionyesha nia ya kutaka kumsajili.

“Ni kweli nimesaini mkataba mpya na Simba wa miaka miwili, tumekubaliana kila kitu na sasa nabakia kikosini kuendelea na majukumu yangu” alisema Mkude.

Hofu ilikuwa imetanda kwa wapenzi na mashabiki wa Simba baada ya kuzagaa kwa tetesi kuwa nahodha huyo alikuwa anakaribia kujiunga na Yanga huku ikifahamika kuwa mshambuliaji Ibrahim Ajib ameshamalizana na mabingwa hao katikati ya juma hili.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *