Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Simba Wawafuata Wababe wa Yanga

0 207

SIMBA imekuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kutinga hatua ya nusu fainali ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kariobangi Sharks kwa penati 3-2.

Related Posts
1 of 32

Mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Afraha jijini Nakuru ilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bila mabao ndipo ilipoamuliwa mikwaju ya penati itoe maamuzi ambapo ushindi wa Simba unawafanya wakutane na Kakamega Home Boys walioitoa Yanga jana.

Simba haikuonyesha kiwango kizuri leo jambo ambalo hata kocha Pierre Lechantre amekiri huku akiahidi kukaa na wachezaji wake ili kuwajenga upya kuelekea mchezo wa nusu fainali.

Michuano hiyo itaendelea tena kesho ambapo Singida United watapambana na AFC Leopards katika mchezo wa mwisho wa robo fainali.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...